Colombia imehitimisha ndoa za utotoni baada ya kampeni ya miaka 17

THE GUARDIAN

Baada ya majaribio manane yasiyo fanikiwa ya kupitisha sheria na mapambano ya miaka 17 kwa ajili ya haki, wabunge wa Colombia hatimaye wameidhinisha mswada wa kuzuia ndoa za utotoni nchini humo, hatua muhimu katika kupambana na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.