Michezo ya Olimpiki ya Vijana yaanza Senegal, ya kwanza barani Afrika

AFRICA NEWS

Michezo ya Olimpiki ya Vijana ilifunguliwa Jumamosi nchini Senegal, tukio la kwanza la Olimpiki barani Afrika. Wanariadha takriban 2,700 wa miaka 14 hadi 17 watashindana hadi Novemba 13 katika mashindano 153 ya medali ya michezo 25, mjini Dakar, Diamniadio na Saly. Timu ya kwanza ya wakimbizi ina wanariadha sita wanaoishi Kenya na Uganda.