
Jaji wa Kenya atangaza kwamba jaribio la kujiua si kosa la jinai
NATION
Katika uamuzi wa kihistoria, jaji wa Kenya ametangaza sehemu ya sheria za jinai nchini inayoharamisha jaribio la kujiua kuwa si ya kikatiba. Amesema kuwa ni ubaguzi kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili yasiyotibiwa ambayo hawawezi kuyadhibiti.