Kasuku wa Kibrazili arejea katika makazi yake ya asili

MONGABAY

Kasuku wa Amazon mwenye mkia mwekundu, ambaye asili yake ni Brazil, aliwahi kuwa miongoni mwa spishi zilizo hatarini kutoweka. Sasa, aina mbili za kasuku hao wanaanzishwa tena porini, na watawekewa vitambulisho miguuni ili kuwalinda dhidi ya biashara haramu ya wanyama.