Miji 19 yapunguza uchafuzi wa hewa kwa zaidi ya asilimia 20

THE GUARDIAN

Kuanzia London nchini Uingereza hadi San Francisco Marekani na Beijing nchini China, miji 19 imepunguza vichafuzi viwili vikuu vya hewa kwa zaidi ya asilimia 20 tangu 2010. Njia za baiskeli, magari ya umeme na vizuizi kwa magari yanayochafua sana vinachangia hewa safi zaidi mijini.