Hungary yafuta vifungu vya sheria vilivyolenga watu wa LGBTQ

BBC

Bunge la Hungary limebadili Sheria ya Ulinzi wa Watoto ya 2021 na kuondoa vifungu vilivyopiga marufuku kuonesha au kuendeleza ushoga na utambulisho wa watu waliobadili jinsia. Wanaharakati wamekaribisha hatua hiyo, lakini wanataka mageuzi zaidi kuhusu ndoa, kuasili watoto na utambuzi wa kisheria.