Katika Bolzano, madaktari bingwa wastaafu hukutana na wakazi mara moja kwa mwezi katika nyumba ya wageni kutoa ushauri wa afya bila malipo wala miadi. Cafe Med haifanyi uchunguzi wala kuchukua nafasi ya matibabu ya kawaida, lakini husaidia hasa wazee kuelewa taarifa zao za kitabibu.

Madaktari wastaafu watoa ushauri bure katika Bolzano
DEUTSCHE WELLE
