Baada ya miaka ya kuendesha kampeni, wanaharakati wa mazingira wanasherehekea uamuzi wa Thailand wa kupiga marufuku uagizaji wa plastiki taka kutoka nchi za kigeni. Hatua hii inatarajiwa kuchochea urejeleaji wa plastiki nchini, kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali na kupunguza kiwango cha takataka za plastiki zisizotumika.