Kiwanda cha Ufaransa chageuza jeans kuwa vihami jengo

FRANCE 24

Kaskazini mwa Ufaransa, kampuni moja inasaga na kuchakata mamilioni ya jeans zilizotupwa kuwa paneli za kuhami majengo dhidi ya baridi na joto. Nyenzo hiyo tayari imetumika katika baadhi ya majengo maarufu nchini humo, ikitoa matumizi mapya ya taka za denim kwenye ujenzi.