Makumbusho pekee ya kugusa nchini Italia yakaribisha wageni wote

DEUTSCHE WELLE

Jumba la makumbusho la Omero jijini Ancona, lililoanzishwa na wanandoa vipofu Aldo na Daniela Grassini miaka ya 1990, ndilo pekee la kugusa linalofadhiliwa na serikali nchini Italia. Wageni hugusa nakala za sanamu za Kirumi na Kigiriki na kichwa cha David wa Michelangelo. Tangu 2012 liko katika Mole Vanvitelliana.