Viota vya kasa loggerhead vyaongezeka baada ya miaka ya uhifadhi

MONGABAY

Utafiti wa miaka 27 umeonyesha ongezeko la mara 80 la viota vya kasa loggerhead katika fukwe tatu za Boa Vista nchini Cabo Verde. Watafiti wanasema mafanikio hayo yametokana na ulinzi wa makazi, doria dhidi ya ujangili, programu za hatchery, ufuatiliaji wa muda mrefu na ushiriki wa jamii.